Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sure boy atoa neno kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na Yanga

Sure Neno Usajili mpya Yanga, Salum Abubakar "Sure boy"

Sun, 26 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amekamilisha dili la kujiunga na Yanga baada ya takribani miaka 14 kuitumikia klabu ya Azam FC.

Baada ya kujiunga na Yanga, Sure Boy ameandika maneno ya kwa kheri Azam, maneno yenye shukrani kwa namna ambavyo wamemlea kwa kipindi chote kuanzia mwaka 2007.

“Assalam Alaykum, nitumie fursa hii kiushukuru Management, Technical Staff, Makocha, Viongozi, Mashabiki, Wachezaji Wenzangu na wafanyakazi wote wa Azam Tuliofanya kazi kwa pamoja kwa Ushirikiano Kwa kipindi kirefu Sana".

Nyakati za huzuni, majonzi Na furaha zote tulisimama pamoja kuipigania Timu Kwa jasho Na damu.

Nimeishi Kama Mwanafamilia kwa miaka yote hapo klabuni, nilikuja nikiwa kijana Mdogo Sana".

Aidha, Salum amesema anaondoka Azam kwenda timu ya Wananchi kutafuta changamoto mpya

“Naondoka kutafuta changamoto mpya nikiwa nimepevuka kimwili na kiakili.

Mimi ni Binaadamu kama kuna eehemu nimewakosea naombeni mnisamehe na mimi pia nimesamehe kama mlinikosea.

Asanteni Sana Azam FC nathamini Mchango Wenu Mkubwa Katika Maisha Na Career Yangu Kwa Ujumla,” amemalizia Sure Boy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live