Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sure Boy ukipenda muite 'Luka Modric wa Avic Town'

Gamondi Sureboy Sure Boy ukipenda muite 'Luka Modric wa Avic Town'

Sun, 17 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ilikuwa ni tarehe 27 August, 2012 pale White Hart Lane aliondoka mtu mmoja na kutua Santiago Bernabeu. Alikuwa ni kijana ambaye alijenga ngome imara chini ya Kocha Harry Redknapp kabla ya kuendeleza ubora wake chini ya bwana mdogo Andre Villas Boas.

Pesa za Don Perez zilimvuta pale Los Blancos, akamaliza hadithi yake ya kuvutia ndani ya EPL kisha akaenda kuanza upya kujitafuta kule La Liga ambako palimshinda Ricardo Kaka. Hata yeye alianza kwa mwendo mbaya hadi ikafikia mashabiki wakamtaja kuwa ni moja kati ya sajili mbovu zaidi za msimu huo (the worst signing of the season) lakini Mourinho aliwaambia mpeni muda, mtatubu.

Ni LUKA MODRIC, moja kati ya viungo bora wa soka barani Ulaya mpaka sasa.

Story haimhusu Modric hii.

Pale Avic Town ukienda mida ya jioni utakutana na Modric mwingine ambaye kiwango chake hakitetereki. Alizaliwa kwenye familia ya mpira, akaishi maisha yake kimpira mpira na sasa ni fundi wa mpira. Huenda wengine wanamuona sasa hivi lakini huyu ni fundi toka kitambo. Mmemjua?..

Ni Salum Abubakary 'Sureboy', the boy is very sure. Kile anachokifanya kila akipewa nafasi ni mwendelezo tu na kuwakumbusha Watanzania kwamba yeye ni yule yule wa jana, leo na kesho. Hatajwi sana kwa sababu sio mtu wa namba namba (takwimu za magoli + assist) lakini ni kiungo bamia.

Zile pasi rula kama za Moussa Dembele wa ile Spurs ya Pochettino, zile penetration passes, jicho la kuona mashimo na njia za boli ni uthibitisho juu ya haya maneno. Surely Sureboy is sure.

Kuna mwenye swali?

Maneno mnayo nyie.. Wa kuponda mnakaribishwa, wenye makasiriko pia mlango upo wazi hapo (picha ya pili) mnaweza kuingia humo mkimaliza mtoke.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live