Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sure Boy nje mwezi mzima

Sure Boy Vs Mtibwa Salum Abubakari ‘Sure Boy’.

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mchezeshaji wa Yanga, Salum Abubakari ‘Sure Boy’ muda wowote atafanyiwa operesheni ya bega ikiwa ni baada ya kupata majeraha hayo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Mchezo huo ulipigwa juzi kwenye Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera ambao ulimalizika kwa suluhu.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Tanzaniaweb.com, kiungo huyo alipata majeraha makubwa ambayo yalimsababishia ashindwe kuendelea na mchezo huo.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kiungo huyo atafanyiwa vipimo maalum na madaktari wa timu hiyo, kabla ya kufanyiwa oparesheni ambayo huenda ikamuweka nje ya uwanja zaidi ya mwezi mmoja.

“Sure Boy yupo chini ya uangalizi hivi sasa wa madaktari ambao wanatarajiwa kumfanyia vipimo kabla ya kufanyiwa operesheni ya bega.

“Hiyo ni baada ya bega lake kuonekana limepata jeraha kubwa, hivyo hivi sasa yupo chini ya uangalizi huku akiendelea na matibabu,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo Meneja wa timu hiyo, Walter Harrison alisema: “Ni kweli Sure Boy alipata majeraha makubwa ya bega, hivyo anatarajiwa kufanyiwa operesheni.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live