Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sure Boy asepa viunga vya Chamazi, Kuungana na Aucho Yanga

Sure Boy Pic Data 1 (600 X 303) Kiungo anaetajwa kutimka Azam FC

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baba mzazi wa Kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amefichua siri kuhusu mwanawe kumalizana na Vinara wa Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans.

Baba Mzazi wa kiungo huyo ‘Abubakar Salum’ ambaye aliwahi kutamba na klabu ya Young Africans, amefunguka kuhusu mpango wa mwanawe, kutokana na tetesi za usajili zinazoendelea katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo.

“Nilianza kusikia kwenye vyombo vya habari lakini tayari kijana mwenyewe amenieleza kila kitu juu ya Yanga, tayari wameshakubaliana vitu vingi na mabosi wa Yanga kwa ajili ya kusaini mkataba baada ya TFF kuuvunja mkataba wake na Azam kutokana na mgogoro wao wa muda mrefu.

“Nadhani kwa sasa watakuwa wamebakisha mambo machache ya kimasilahi kabla ya kumalizana kabisa, suala ya yeye kwenda kwenye timu ambayo nilicheza kwangu ni jambo zuri japokuwa sikutaka iwe hivyo, ila kutokana na matatizo yake na Azam imekuwa ni jambo kubwa.”

“Yanga kuna wachezaji wengi wazuri, suala la yeye kucheza itategemea na mwalimu atatumia mfumo gani, ila naamini atacheza tu,”

‘Sure Boy’ alisimamishwa na Uongozi wa Azam FC kwa muda usiojulikana, kufuatia tuhuma za utovu wa nidhamu sambamba na wenzake Mudathir Yahya na Agrey Morris.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live