Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sure Boy, Morris Wapigwa Stop Azam

AGGREY Aggrey Morris (kushoto) akiwa na mtendaji mkuu wa Azam Abdulkarim Amin

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Wachezaji waandamizi wa Azam, viungo Salum Aboubakar ‘Sure Boy’, Mudathir Yahya na beki Aggrey Morris wamesimamshwa na uongozi wa timu hiyo kwa muda usiojulikana huku wakishindwa kujua makosa yao.

Ni zaidi ya mwezi sasa tangu wachezaji hao wasimamishwe kufuatia kupewa barua ambazo zinadai wamesimamishwa kwa muda usijulikana bila ya kuelezwa makosa yao.

Mmoja kati ya wachezaji hao ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, amesema kuwa mpaka sasa hawajui kwa nini wamesimamishwa kwa muda usiyojulikana kwa kuwa hakuna walipoelezwa makosa yao.

“Ni mwezi sasa tangu tusimamishwe na kifupi hakuna ambaye anajua kati yetu ni kwa nini labda tumesimamishwa yaani unavyoona huko mitandaoni watu wakiongea na sisi tunaona hivyo hivyo hatujui chochote na hakuna ambaye kati yetu anajua sababu ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana,” amesema mchezaji huyo.

Championi lilimtafuta ofisa habari wa timu hiyo, Thabith Zakaria ‘Zaka Zakazi’ lakini hakuweza kupatikana kutokana na simu yake kuita muda mrefu bila ya kupokelewa.

Chanzo: globalpublishers.co.tz