Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sure Boy: Mimi Siwezi Kukosa Nafasi Yanga

Sure Neno Sure Boy: Mimi Siwezi Kukosa Nafasi Yanga

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KIUNGO mpya wa Yanga, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amevunja ukimya juu ya nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha timu hiyo kwa kusema yeye ni mchezaji mkubwa, hawezi kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza, lakini kocha Nasreddine Nabi ndiye anayejua atakapompanga kucheza.

Kiungo huyo amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam ambayo ilikuwa imempa adhabu ya kumsimamisha kwa muda usiojulikana akiwa na wenzake, Mudathir Yahaya na Aggrey Morris.

Sure Boy juzi Jumatano alianza mazoezi rasmi na timu hiyo baada ya kutambulishwa tayari kwa kuanza majukumu mapya.

Sure Boy alisema kuwa anashukuru amepokelewa vizuri na wachezaji wenzake ndani ya timu hiyo ambao kwake hakuona ugeni wowote kutokana wengi wao kukutana nao kwenye timu ya Taifa ukiondoa wachezaji wa kigeni.

“Nashukuru jana (juzi) nimeanza mazoezi na timu, kitu kikubwa ni kwamba wamenipokea vizuri, wapo ambao ni wadogo zangu na wapo ambao nimekuwa nikikutana nao kwenye timu ya taifa labda kwa wachezaji wa kigeni ambao nao wamenipokea vizuri jambo ambalo naamini litaongeza chachu ya kutaka kufanya makubwa kwenye ligi.

“Suala la nitacheza wapi hilo kwangu naona ni dogo kwa sababu mimi ni mchezaji mkubwa, nimeshacheza ligi kwa misimu 13 halafu nina uzoefu wa kutosha hivyo siwezi kuwa na presha ya nafasi ya kucheza kama watu wanavyofikiria lakini bado naamini mwalimu mwenyewe atakuwa anatambua ni nafasi gani naweza kucheza bila ya kujali viungo waliopo, mbona hata Azam kulikuwa na wachezaji kibao wakali na nilikuwa nikicheza,” alisema Sure Boy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live