Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sure Boy: Kucheza Yanga kuna maana kubwa

7b701041bc402517951adcf47fd1eaaa.jpeg Salum Abubakary ‘Sure Boy’

Mon, 27 Dec 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kiungo mpya wa Yanga, Salum Abubakary ‘Sure Boy’ amesema kujiunga na timu hiyo kuna maana kubwa kwake.

Aidha, amesema lengo lake kubwa kwa sasa ni kushirikiana na wachezaji wenzake ili kutimiza malengo ya klabu hiyo kubeba mataji yote msimu huu.

Sure Boy tayari ametambulishwa na Yanga baada ya kumalizana na timu yake ya Azam FC ambayo ameitumikia kwa zaidi ya misimu 14.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sure Boy alisema anajua timu aliyo jiunga nayo ina ushindani mkubwa wa namba na nafasi anayocheza kuna wachezaji wengine bora na wanafanya vizuri lakini atapambana mazoezini ili kumshawishi kocha kumpa nafasi.

“Nimejiunga na timu yenye presha kubwa kuanzia malengo iliyonayo lakini pia kucheza

Yanga unatakiwa kuwa fiti vinginevyo unaweza kujikuta unapotea, binafsi nimejipanga kukabiliana navyo vyote nikishirikiana na wachezaji wengine naamini tutafanikiwa,” alisema Sure Boy.

Kiungo huyo alisema asilimia kubwa ya wa chezaji wa Yanga ni rafiki zake na huwa wanakutana timu ya taifa kwa hiyo hakuna ugumu kwake sababu mpira ni ule ule cha msingi ni kutekeleza kile anachoelezwa na kocha.

Alisema anajisikia furaha kubadilisha mazingira na amejipanga kuhakikisha anatoa mchango wake ili kusaidia timu ifikie malengo ambayo imekusudia msimu huu.

Sure Boy amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam FC ambako aliomba kuvunja mkataba wake kutokana na kutaka kubadili mazingira ya kazi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz