Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sure Boy Agomea Mazoezi Azam

Sure Boy Pic Data 1 (600 X 303) Sure Boy Agomea Mazoezi Azam

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya Kocha Mkuu anayeishikilia Azam kwa muda, Mmarekani Abdihamid Moallin kuomba kwa wakongwe Aggrey Morris, Salum Aboubakar Sure Boy na Mudathiri Yahaya, ambao walisimamishwa kwa makosa na utovu wa nidhamu kurejea kambini, Sure Boy yeye kaweka mgomo.

Inaelezwa kuwa Sure amesaini kwenye klabu ya Yanga, lakini hana baraka zote kutoka kwenye uongozi wa Azam FC.

Chanzo cha ndani kinasema kuwa wachezaji wengine wamekubali kurejea klabu hapo, lakini Sure amegoma.

“Mudathir na Aggrey wenyewe wataanza mazoezi na wenzao (kesho) baada ya kocha mkuu wa muda kuomba warudishwe kikosini ila kwa Sure Boy imekuwa ngumu kukubali, na ameshawaaambia rafiki zake kuwa hatakwenda.

“Mpaka jana Jumamosi na leo Jumapili Sure alikuwa amekataa kabisa kuweza kurejea Azam ingawa wenyewe Azam nao wanasikia kuwa amesaini Yanga lakini wenyewe hawajatoa baraka zote,” kilisema chanzo hicho cha uhakika.

Alipotafutwa kiungo huyo alisema kwa ufupi: “Mambo, sijui chochote na siwezi kuzungumza kitu kwa sasa asante.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live