Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sura mpya za kazi kwenye vikosi vya Ligi Kuu England msimu huu

Decline Rice Injury Decline Rice

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Dirisha la usajili wa wachezaji la majira ya kiangazi la mwaka huu kwa England lilifunguliwa Juni 14 na litafungwa rasmi Septemba Mosi, 2023. Wachezaji wasiokuwa na klabu wanaweza kusajiliwa muda wowote, klabu inaweza kusajili kwa mkopo pia kulingana na kanuni zilizopo kwenye ligi husika na klabu inaweza kumsajili kipa kwa dharura kama hawatakuwa na kipa chaguo la kwanza kwenye kikosi chake.

Kwenye Ligi Kuu England klabu zimeshafanya dili kadhaa za kuleta mastaa matata kabisa katika kuboresha vikosi vyao ikiwamo usajili wa Pauni 100 milioni uliowahusu wakali kama Declan Rice, aliyeenda Arsenal na Moises Caicedo, aliyetua zake Chelsea. Kutokana na hilo, hii hapa orodha ya usajili uliokamilika wa mastaa wapya kwenye kila kikosi cha Ligi Kuu England kwa msimu huu wa 2023-2024.

ARSENAL

Wapya: Kai Havertz (Pauni 65milioni, Chelsea), Jurrien Timber (Pauni 34.3milioni, Ajax), Declan Rice (Pauni 100milioni, West Ham), David Raya (mkopo, Brentford).

ASTON VILLA

Wapya: Youri Tielemans (bure, Leicester City), Rico Richards (bure, West Brom), Pau Torres (Pauni 27.77milioni, Villarreal), Moussa Diaby (Pauni 34.6milioni, Bayer Leverkusen), Nicolo Zaniolo (mkopo, Galatasaray).

BOURNEMOUTH

Wapya: Tyler Adams (Pauni 23milioni, Leeds United), Hamed Traore (Pauni 20milioni, Sassuolo), Justin Kluivert (Pauni 9.5milioni, Roma), Romain Faivre (Pauni 12.8milioni, Lyon), Milos Kerkez (Pauni 15.5milioni, AZ Alkmaar), Ionut Radu (mkopo, Inter Milan), Max Aarons (Pauni 8milioni, Norwich), Alex Scott (Pauni 20milioni, Bristol City).

BRENTFORD

Wapya: Mark Flekken (Pauni 11milioni, Freiburg), Ethan Brierley (ada imefichwa, Rochdale), Kevin Schade (Pauni 22milioni, Freiburg), Ji-soo Kim (Pauni 550,000, Seongnam), Romeo Beckham (ada imefichwa, Inter Miami), Nathan Collins (Pauni 23milioni, Wolves).

BRIGHTON

Wapya: Joao Pedro (Pauni 30milioni, Watford), James Milner (bure, Liverpool), Mahmoud Dahoud (bure, Borussia Dortmund), Bart Verbruggen (Pauni 16.3milioni, Anderlecht), Igor (Pauni 14.5milioni, Fiorentina)

BURNLEY

Wapya: Jordan Beyer (Pauni 13milioni, Borussia Monchengladbach), Michael Obafemi (Pauni 3milioni, Swansea), Dara O’Shea (Pauni 7milioni, West Brom), Zeki Amdouni (Pauni 16.15milioni, FC Basel), James Trafford (Pauni 14milioni, Man City), Nathan Redmond (bure, Besiktas), Luca Koleosho (Pauni 2.6milioni, Espanyol B), Jacob Bruun Larsen (mkopo, Hoffenheim), Sander Berge (Pauni 15milioni, Sheffield United), Wilson Odobert (Pauni 10.36milioni, Troyes), Hannes Delcroix (Pauni 2.5milioni, Anderlecht), Aaron Ramsey (Pauni 14milioni, Aston Villa).

CHELSEA

Wapya: Christopher Nkunku (Pauni 52milioni, RB Leipzig), Nicolas Jackson (Pauni 31.7milioni, Villarreal) Diego Moreira (bure, Benfica), Alex Matos (bure, Norwich), Angelo (Pauni 13milioni, Santos), Lesley Ugochukwu (Pauni 23milioni, Rennes), Axel Disasi (Pauni 38.7milioni, Monaco), Robert Sanchez (Pauni 25milioni, Brighton), Moises Caicedo (Pauni 100milioni, Brighton), Romeo Lavia (Pauni 53milioni, Southampton).

CRYSTAL PALACE

Wapya: Jefferson Lerma (bure, Bournemouth), Matheus Franca (Pauni 17milioni, Flamengo).

EVERTON

Wapya: Ashley Young (bure, Aston Villa), Arnaut Danjuma (mkopo, Villarreal), Chermiti (Pauni 13milioni, Sporting Lisbon), Jack Harrison (mkopo, Leeds).

Chanzo: Mwanaspoti