Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Super League – Klabu zaingia mchecheto Ulaya

Arton150017 Super League – Klabu zaingia mchecheto Ulaya

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Mkurugenzi Mtendaji wa Super League, Bernd Reicart amesisitiza kwamba klabu zote za Ulaya zinaogopa vitisho vya UEFA ikishinikiza zisiunge mkono mashindano hayo kuanzishwa.

Hiyo ni baada ya mahakama ya haki kupitisha rasmi ujio wake, hivyo UEFA na FIFA haziwezi kuzuia mashindano hayo.

Timu mbili tu ndo ziliunga mkono mashindano hayo tangu mwaka 2021, nazo ni Real Madrid na FC Barcelona, lakini timu za Atletico Madrid, Paris Saint-Germain, Juventus, Bayern Munich ni miongoni zinazopiga michuano ya Super League kuanzishwa.

Lakini bosi huyo anaamini kuwa baadhi ya klabu zinaogopa kujitokeza kuunga mkono mashindano haya mapya na alisema: “Pendekezo hili la hivi punde la Super League limefichuliwa na mchango wa klabu nyingi, tumezungumza na klabu nyingi katika miezi ya hivi karibuni. Lakini klabu hizi zinaogopa kuonekana kujitokeza hadharani kwa sababu ya vitisho. Vilabu vingi vinaunga mkono mradi huu.

“Klabu zimekuwa chini ya ukiritimba kwa miaka 70, udikteta ngumi ya chuma, tunapaswa kubadili hili, ni kawaida kwamba wengine huchukua muda mrefu na wengine muda mfupi, lakini ni fursa nzuri kwa klabu kusimamia mustakabali wao.”

Bosi huyo alipoambiwa uvumi kwamba klabu kutoka Saudi Arabia zinaweza kualikwa kujiunga na Super League, akafafanunua zaidi: “Klabu za Saudi Arabia katika Super League? Hakutakuwa na klabu ambazo hazipo Ulaya, klabu zitakazoshiriki za Ulaya tu.”

Man United ilitoa tamko lake rasmi lililosomeka hivi: “Uamuzi wetu hautabadilika, tumebaki kujitolea kushiriki michuano ya UEFA na tutashirikiana na UEFA bega kwa bega. Ligi Kuu England, pamoja na wenzetu tunaunga mkono UEFA kwa ajili ya maendeleo ya soka Ulaya.”

Nayo klabu ya Atletico ilisema: “Familia ya soka Ulaya haiitaki Super League.

Chanzo: Dar24