Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sumaye aeleza alivyotumwa na Mkapa ujenzi wa uwanja

SUMAYE UWANJA WA MKAPA Sumaye aeleza alivyotumwa na Mkapa ujenzi wa uwanja

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ameeliza jinsi Hayati Benjamini Mkapa alivyomtuma China kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Sumaye ameyasema hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na Cluds FM, leo Mei 31, 2023.

“Suala la ujenzi wa uwanja [Benjamin Mkapa Stadium] tulilijadili sana mimi na Mzee Mkapa, akanituma kwenda China kuongeanao ili watusaidie kujenga huo uwanja.”

“Nilifika China tukaongea na Waziri Mkuu wao, badae Waziri wao wa mambo ya Michezo akaja huku [Tanzania] tukajadili sana.”

“Kwa hiyo ni wazo ambalo Mzee Mkapa alikuwanalo na tukasaidiana kuhakikisha uwanja unajengwa. Aliniambia nisimamie hilo jambo kwa kushirikiana na Mawaziri waliokuwepo wakati ule.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live