Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sugu atangaza kununua goli la Mbeya City kwa Mil. 1

MBEYA CITY KUSHUKA DARAJA Sugu atangaza kununua goli la Mbeya City kwa Mil. 1

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini na Mkongwe wa muziki wa Hip Hop Bongo, Joseph Mbilinyi 'Sugu' ametangaza kuisapoti timu ya nyumbani kwao Mbeya City kwa kununua goli kwa shilingi Milioni 1.

Sugu ametangaza jambo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo amesema, amefanya hivyo ili kuinusuru timu hiyo isishuke daraja.

"Mbeya City Stand Up!! Timu yetu iko hatarini kushuka daraja, TUSIKUBALI! Tumebakiza mechi 4 na ili kupona inabidi tushinde hata mechi 2 tu… Katika kuhamasisha Wachezaji wetu uwanjani, Mimi nitatoa 1M kwa kila GOLI la USHINDI kwenye mechi zote zilizobaki na mkwanja utaenda kwa Mfungaji…"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live