Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Subirini kwenye hawa mmoja anatua

Sl Benfica V Burnley Fc Pre Season Friendly Joao Neves

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal kwa sasa inadaiwa kuwa bize kuhakikisha inampata mbadala wa Thomas Partey anayedaiwa atakuwa nje hadi kukaribia mwishoni mwa msimu kutokana na majeraha yanayomuandama.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta na benchi lake la ufundi wanajaribu kuangalia mbadala wake na ripoti zinadai kuna wachezaji watano ambao mmoja wao huenda akasajiliwa katika dirisha lijalo. Hawa hapa ni mastaa watano ambao mmoja wao anaweza kutua Arsenal kwa mujibu wa ripoti mbalimbali.

Martin Zubimendi

Mwaka huu Real Sociedad imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora kwa mara ya kwanza katika historia yake na kwa kiasi kikubwa Zubimendi alichangia suala hili.

Staa huyu mwenye umri wa miaka, 24, amekuwa akifananishwa sana na staa wa zamani wa Barcelona, Xavi.

Hadi sasa amecheza mechi mbili za kimataifa akiwa na Timu ya Taifa ya Hispania na anatajwa kuuzwa kwa bei rahisi jambo ambalo linaweza likaishawishi zaidi Arsenal.

Hata hivyo, kunaweza kuwa na ushindani kwani Kocha Bayern Munich ameonyesha nia ya kutaka kumchukua kiungo huyu ambaye amewahi kushinda taji la Copa del Rey mwaka 2020.

Ruben Neves

Kwa hapa ni ngumu Arsenal kutoa pesa ya kumnuna na kumlipa mshahara sawa na anaolipwa kwa sasa na Al Hilal huko Saudi Arabia kwa sababu sheria za usawa matumizi zitawabana.

Newcastle ndiyo ilikuwa timu yakwanza kutajwa katika siku za hivi karibuni kwamba inafikiria kumrudisha staa huyu wa kimataifa wa Ureno, England lakini mpango wao huenda ukaharibiwa kwa sababu timu ya Nevez na yao zote zinamilikiwa na Saudi Arabia’s Public Investment Fund (PIF), na itakapofika Januari timu za Ligi Kuu England zimepanga kupiga kura za kuzuia timu zinazomilikiwa na timu za ligi hiyo kuchukua ama kutoa wachezaji kwa mkopo ikiwa mmiliki wa timu husika anamiliki hiyo timu nyingine.

Hiyo inaweza kuipa uhuru Arsenal wa kumpata staa huyu mwenye umri wa miaka 26.

Amadou Onana

Alikuwa akihusishwa sana na Arsenal mwaka jana. Staa huyu wa kimataifa wa Ubelgiji alijiunga na Everton akitokea Lille kwa ada ya uhamisho ya Pauni 33 milioni mwaka 2022 na tangu hapo amekuwa mmoja kati ya wachezaji wachache wa Arsenal wanaofanya vizuri kwenye kikosi cha Sean Dyche.

Inawekana ikawa ngumu kumshawishi Sean kwa sababu ndio moja ya silaha anazozitegemea lakini hali ya kiuchumi ya timu hiyo kwa sasa inaweza ikachangia mabosi wao kukubali kumuuza ili kutumia pesa kufanya usajili kwenye dirisha lijalo na kuendesha timu.

Andre

Inawezekana ikawa ngumu pia kwa Arteta kwa sababu staa huyu hajawahi kucheza soka barani Ulaya, lakini kiwango chake kinamuonyesha kuwa ni mmoja kati ya wachezaji hatari kutoka Brazil.

Kiungo huyu aliisaidia Fluminese kushinda taji la Copa Libertadores mwaka huu na pia ameichezea Timu ya Taifa ya Brazil.

Kiwango chake kimesababisha timu nyingi barani Ulaya ikiwemo Liverpool ambao wanadaiwa kutuma wawakilishi wao mara kadhaa kwenda kumtazama akiwa anacheza.

Mkataba wake unamalizika mwaka 2026.

Joao Neves

Ana umri wa miaka 19 tu, lakini ameshaanza kuzivutia timu mbalimbali barani Ulaya.

Staa huyu wa kimataifa wa Benfica ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika timu hiyo na tayari ameshashinda taji la Ligi Kuu Ureno akiwa na wababe hao. Hata hivyo, haijajulikana ikiwa Mikel Arteta atatamani kucheza kamali ya kumsajili mchezaji huyo ambaye hana uzoefu wa kutosha na hatua kubwa za ushindani wakati huu ambao timu inapambana kuhakikisha inashinda taji la Ligi Kuu England, ingawa hata asiposajiliwa na Arsenal kuna uwezekano akaondoka mwishoni mwa msimu kwa sababu timu nyingi zinamhitaji.

Chanzo: Mwanaspoti