Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera 'Robertinho' amesema anajivunja kufanya sub ambazo zimempa ushindi wa 2-1 dhidi ya Singida FG.
Mbungi hiyo ilikuwa live leo Oktoba 8, 2023 katima uwanja wa CCM Liti mkoani Singida ambapo magoli ya Simba yalifungwa na Saidi Ntkbanzokiza na Moses Phiri huku goli la kufutia machozi la Singida likifungwa na Deus Kaseke.
Akizungumzia mchezo huo, Robertinho alisema, anajivunia kufanya mabadiliko kipindi cha pili ambayo yalimlipa na kuweza kupata ushindi huo muhimu ugenini.
"Nilifanya mabadiliko kipindi cha pili ambayo kwa kweli najivunia yametulipa, tumeweza kupata ushindi huu muhimu. Sio rahisi kushinda mechi mbili za ugenini mfululizo hivi lakini Simba ina malengo yake, kucheza vizuri na kushinda," alisema Robertinho.
Wachezaji walioingia kipindi cha pili kwa Simba ni Moses Phiri, Jean Baleke, Israel Mwenda, Sadio Kanoute na Luis Miquissone ambao walichukua nafasi za Clatous Chama, Saidi Ntibanzokinza, Kibu Denis, Mzamilu Yassin na John Bocco.
Simba sasa ipo kileleni ikiwa na alama 15, ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 13 huku Yanga akiwa nafasi ya tatu na alama 12.