Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sub za Gamondi kama za Nabi tu!

Nabi Gamondi 2 WA0002 Sub za Gamondi kama za Nabi tu!

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Nasreddine Nabi wakati akiifundisha Yanga SC alikuwa akifanya tu mabadiliko ujue ni mtego huo unanasa mapema.

Kocha Miguel Gamondi kwenye michezo miwili ya mwisho, sub alizofanya zimewatesa watu wakimemo Simba Sc.

Kwenye mechi dhidi ya Simba, Gamondi alifanya sub ya kumtoa mshambuliaji wake, Kennedy Musonda na kumuingiza Clement Mzize. Mzize touch yake ya kwanza anatoa assist kwa Nzengeli.

Ndani ya dk 6 tu tangu aingie Mzize akatengeneza assist 2, na bado akawapima umri akina Mohammed Hussein na Che Malone. Sub ya Mzize ilienda kuleta chachu ya ushindi, na Simba wakalala yo kwa bao 5.

Kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union kocha alimtoa Musonda anamuingiza Mzize, kocha akamtoa Mudathir Yahya na kumuingiza Jesuz Moloko. Touch ya kwanza ya Moloko akatoa assist kwa Mzize na kufunga goli muhimu, header kama Ronaldo.

Kwa maana hiyo kwenye hizi mbili Yanga imefunga jumla ya magoli 6.

Magoli 4 kati ya 6 wamehusika wachezaji waliotokea sub.

✔Mzize akitokea benchi kafunga 1 na Assist 2

✔Moloko akitokea benchi, assist 1.

Gamondi akifanya mabadiliko ni mtego kama Nabi tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live