Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Suarez amwachia msala Nunez

Suarez X Nunez Suarez amwachia msala Nunez

Mon, 9 Sep 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati anastaafu soka la kwa upande wa timu ya taifa, straika wa zamani wa Liverpool na Barcelona na timu ya taifa ya Uruguay, Luis Suarez amemwambia staa wa Liverpool, Darwin Nunez athibitishe kuwa yeye ni mchezaji bora kwa kuitendea haki nafasi yake.

Nunez kwa sasa anaonekana kuwa atakuwa ndio straika tegemeo katika safu ya ushambuliaji ya Uruguay eneo ambalo Suarez alikuwa akiaminika zaidi.

Staa huyu wa Liverpool ambaye atakosa michezo mitano baada ya kufungiwa kutokana na kufanya vurugu katika michuano iliyopita ya Copa America, atakuwa na kazi ya kuthibitisha hilo mara tu atakapomaliza adhabu yake.

Nunez alifanya vurugu katika mchezo wa nusu fainali ambao ulimalizika kwa Uruguay kupoteza dhidi ya Colombia na mara baada ya mechi kuisha alionekana akienda jukwaani kupigana na baadhi ya mashabiki wa timu pinzani.

"Tayari nilizungumza na Darwin mara baada ya kufungiwa. Wakati mwingine watu hufurahia zaidi unapokuwa chini na kuanguka, lakini watu huumia wanapoona unafanikiwa au kuinuka, na hicho ndicho anachotakiwa kufanya, anatakiwa aamke na kuendelea kuonyesha ubora wake, hivyo ndivyo wanavyofanya wachezaji wakubwa waliokomaa kiakili na kuwaumbua wale watu wanaopenda kumuona akianguka."

Nunez amefunga mabao 13 katika mechi 29 za michuano mbalimbali tangu aanze kuichezea Uruguay na anatarajiwa kuendeleza pale ambapo mastaa kama Suarez na Edinson Cavani walipomwachia.

Suarez ambaye pia aliwahi kuichezea Atletico Madrid alitangaza kustaafu kucheza mechi za kimataifa mapema wiki hii akisema hizi sio nyakati rahisi kwake.

Staa huyu alifurahisha mashabiki wa Uruguay baada ya kucheza mchezo wake wa mwisho uliomalizika kwa suluhu uliopigwa huko Montevideo.

Chanzo: Mwanaspoti