Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Suarez agoma kuwaomba radhi Afrika kwa tukio hili!

Luis Surez Jeuri Suarez agoma kuwaomba radhi Afrika kwa tukio hili!

Thu, 1 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay, Luis Suarez amesema kuwa kamwe hawezi kuomba radhi kwa Ghana kutokana na kitendo chake cha kuzuia goli kwa mkono katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchi Afrika ya Kusini.

Suarez amesema angeomba radhi kama tu, angemjeruhi mchezaji lakini Ghana wenyewe walipata mkwaju wa penati na mchezaji wao akakosa.

Nakuongeza kuwa alisherehekea kitendo cha Ghana kukosa penati kama vile wangefunga goli kama si tukio alilofanya na wangeondolewa katika michuano.

“Siwezi kuomba radhi kwakuwa kadi nyekundu sikupata kwa kumjeruhi mchezaji wa Ghana bali nilizuia mpira usiingie wavuni kwetu na niliadhibiwa, mimi sikukosa penati, aliyekosa ni Mchezaji wa Ghana.”

Nyota huyo amesema hayo wakati timu yake ya Uruguay ikijiandaa kukabiliana tena na Ghana hapo kesho kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia nchini Qatar kuwania kufuzu kwa hatua ya 16 Bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live