Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Suarez: Mimi, Messi na Neymar hatukutaka kushindana

Messi Neymar Suarez Suarez: Mimi, Messi na Neymar hatukutaka kushindana

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez amesema kuwa wakati anakwenda kwenye klabu hiyo watu walidhani kuwa hataweza kufanya vizuri pengine angefunikwa na vivuli vya mastaa kama Lionel Messi na Neymar Jr.

Suarez ambaye ni Raia wa Uruguay amesema kuwa, baada ya kutua Camp Nou alikubaliana na wenzake kushirikiana kwa ajili ya timu badala ya kupambana wao kwa wao.

Utatu huo ulikuwa tishio kwa Ligi Kuu ya Hispania (Laliga) pamoja na michuano mbalimbali ya Ulaya huku wakipewa jina la MSN (Messi, Suarez na Neymar).

"Nilipofika Barcelona, ​​​​nilifika kama nyota huku Neymar na Messi wakiwa tayari. Watu walikuwa wakisema kuwa nyota 3 pamoja hazitafanya kazi. Hatukushindana sisi kwa sisi. Hatukutaka kufanya kitu kingine chochote isipokuwa kushinda na kucheza vizuri pamoja.

"Katika mikwaju ya penalti, Messi alikuwa wa kwanza, kisha Neymar na mimi tulikuwa wa mwisho, lakini tulikuwa wajanja katika kugawana na kutoka hapo ushirikiano ulianza na kuendelea hata nje ya uwanja, na hii ni muhimu sana. Tumefanikiwa kila kitu pamoja,“ amesema Suarez.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live