Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Suala la waamuzi liko hivi

Tatu Malogo Refa Mwamuzi Tatu Malogo

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Matukio yanayoendelea juu ya makosa ya waamuzi yamewafanya wadau wa soka nchini kwa nyakati tofauti kuamini kuwa kasoro hizo zinaondoa ladha ya mashindano husika.

Yapo matukio mengi msimu huu ambayo yameibua mijadala mitanadaoni, likiwamo la mchezo wa Ligi Kuu kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Azam FC, wakati beki wa Wanalambalamba, Lusajo Mwaikenda kufunga akiwa hajaotea, lakini bao lake kukataliwa.

Hayo yaliendelea zaidi baada ya mwamuzi Tatu Malogo na msaidizi wake namba mbili, Abdallah Mkende wa mechi ya Ligi Kuu kati ya Singida Fountain Gate na Simba kuzua sintofahamu mkoani Singida.

Wadau wa soka wengi wameonyesha kutoelewa waamuzi hao kushindwa kutafsiri sheria hasa bao la mchezaji wa Singida, Duke Abuya alilofunga dakika ya 59 kukataliwa baada ya kuonyesha aliotea.

Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Nassor Hamduni alisema wao kama kamati wamewatoa waamuzi hao na sasa wapo chini ya Bodi ya Ligi (TPLB), ambao ndiyo wanaopewa ripoti baada ya mchezo.

Hamduni alisema waamuzi wote ambao wapo kwenye Ligi Kuu ripoti zao huchukuliwa na makamishna wa michezo na kupeleka TPLB, hivyo ni ngumu kwao kujua wapi kuna changamoto na kutoa uamuzi.

"Sisi tunatoa waamuzi kwa Bodi ya Ligi na wanakuwa chini yao na ripoti baada ya mchezo huwa inaenda kwao, lakini sisi kama kamati sasa tukiona makosa yanazidi sasa tunawaondoa katika ratiba;

"Ngumu kukubali mwamuzi akosee mikoa miwili halafu ukaendelea kumpa mechi inakuwa si sawa," alisema Hamduni.

Kwa upande wake, mwamuzi wa zamani, Ibrahim Kidiwa alisema makosa ambayo yanatokea kwa sasa yanaondoa ladha ya soka, akiwataka waamuzi kusome sheria kikamilifu.

Kidiwa alisema sababu ni kutojua vizuri kutafsili sheria na si kitu kingine, kwa sababu kusoma sheria makosa yanayotokea hayawezi kuendelea.

"Upande wa utimamu mimi najua wote wapo vizuri kwa sababu wanatumiwa mazoezi ya kufanya ili wawe bora, unaweza ukawa na mbio nyingi lakini ukawa haujui sheria vizuri kwahiyo ni tatizo.

"Ifike muda wawe wanauliza hata waamuzi wa zamani wanaweza kuwasaidia katika sheria," alisema mwamuzi huyo kutoka Tanga.

Chanzo: Mwanaspoti