Sat, 8 Jun 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mwaka 2020, Barcelona waliamua kuachana na Luis Suárez tena, kwa hivyo wakamuuza kwa Atlético Madrid kwa pauni milioni 6.5 tu, Kocha Ronald Koeman ndiye aliyempa taarifa hizo kupitia simu.
Suarez ambaye kwa sasa anakipga Inter Miami anasimulia: "Simu kutoka kwa Koeman kuniambia kuwa hakunihitaji ilidumu kwa sekunde 40, sio njia ya sahihi ya kumwambia legend.
“Kwanza, aliniambia kuwa sikuwa katika mipango yake na kisha akaniambia kwamba ikiwa sitatatua ishu ya mkataba wangu nitacheza dhidi ya Villarreal. Hakuwa na utu wa kuniambia mambo waziwazi, kama hakunitaka au ikiwa ni klabu ambayo haikunitaka.”
Chanzo: www.tanzaniaweb.live