Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika mpya Simba na jezi namba 9 yenye gundu?

Nani Kumpisha Pa Omar Jobe Straika mpya Simba na jezi namba 9 yenye gundu?

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imemtambulisha mshambuliaji wake mpya, Pa Omar Jobe ambaye kwenye picha zake za huko alikokuwa akicheza anaonekana kupendelea kuvaa jezi namba tisa ambayo imekuwa ikigomewa na mastaa wengi ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi ikitafsiriwa kwamba ina gundu klabuni hapo.

Mara ya mwisho jezi namba tisa ndani ya kikosi cha Simba ilivaliwa na mshambuliaji raia wa Burundi, Laudit Mavugo ambaye hakufanya vizuri ndani ya kikosi cha Simba na baadaye kupewa mkono wa kwaheri.

Mshambuliaji huyo mpya wa Simba kutoka klabu ya FC Zhenis Astana ya Ligi Kuu ya Kazakhstan, Jobe atafuata nyayo za mastaa waliopita hivi karibuni na kuikataa jezi hiyo au atavaa kama ilivyokuwa kwa mastaa hawa?

ZAMOYONI MOGELLA - SIMBA Anatajwa kuwa mmoja wa washambuliaji hatari zaidi kuwahi kutokea nchini aliyecheza timu zote mbili za Simba na Yanga, lakini Msimbazi ndiko alikocheza kwa mafanikio makubwa kutokana na kucheza misimu mingi, huku Yanga akiitumikia msimu mmoja na kuamua kutundika daluga.

“Imani tu ndio zinawaharibu wachezaji, mimi nimecheza Simba kwa mafanikio na jezi hiyohiyo namba tisa na nilikuwa nafunga sana. Nakumbuka niliikuta inavaliwa na mtu sikumbuki nani, lakini kutokana na umahiri wangu wa kufunga nikapewa tisa,” anasena na kuongeza kuwa, “sina kumbukumbu nilifunga mabao mangapi ila nilikuwa imara sana eneo hilo.”

EDWARD CHUMILA - SIMBA Aliingia Simba kuziba nafasi ya Mogella baada ya straika huyo kupata nafasi ya kwenda Uarabuni kucheza soka la kulipwa na alikabidhiwa jezi namba tisa na kugeuka kuwa kipenzi cha wana Msimbazi kutokana na kuwafunga watani wao Yanga mara kwa mara.

WILKER DA SILVA - SIMBA Mwaka 2019, Simba iliwasajili Wabrazili watatu akiwamo straika Wilker da Silva aliyedumu kwa msimu mmoja tu baada ya kushindwa kufanya vizuri. Da Silva aliyekuwa anavaa jezi namba tisa hakupata muda wa kutosha kucheza kutokana na majeraha ya mara kwa mara.

BETRAM MWOMBEKI -SIMBA Mwaka 2013, Betram Mwombeki baada ya kutua katika kikosi cha Simba kutokea Marekani alikuwa akivaa jezi namba tisa ila ghafla alibadilisha na kuvaa 23.

HENRY JOSEPH - SIMBA Mwaka 2013 baada ya kurejea nchini kutoka Norway alikokuwa anacheza soka, nahodha wa zamani wa Simba, Henry Joseph alijiunga na timu Wekundu wa Msimbazi na alitakiwa kuvaa namba tisa.

Joseph aliwaambia viongozi Simba hakuwa tayari kuvaa jezi hiyo kutokana na mambo mawili.

“Kwanza niliwaambia wakati naondoka Simba nilikuwa navaa jezi namba sita na ndio chaguo langu, kama hiyo inavaliwa na mchezaji mwingine na hayupo tayari kuniachia basi nitafanya chaguo jingine,” anasema Joseph.

“Nikawaambia wanipe jezi kati ya namba 12 au 14 naweza kuvaa, lakini hiyo namba tisa siyo chaguo langu na wala hainivutii kuvaa, lakini mastraika ndio wakivaa inakuwa sawa, tulikubaliana na nikaiacha.”

GERVAS KAGO - SIMBA Jezi namba tisa ya Simba kwa mwaka 2011 ilikuwa ikivaliwa na Gervas Kago aliyesajiliwa kutoka Jamhuri ya Kati. Lakini maisha yake kikosini hayakuwa katika kiwango bora.

BLAGNON/MAVUGO - SIMBA Baada ya kuwasili nchini 2016 kumalizana na Simba, mshambuliaji raia wa Burundi, Laudit Mavugo aliomba jezi namba tisa. Wakati huo ilikuwa inavaliwa na Blagnon Frederick kutoka Ivory Coast ambaye Simba ilimtoa African Sports ya Abidjan. Mavugo na Blaignon wote walishindwa kufanya vizuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live