Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Yanga atupia "Hat trick" michuano U20

D0BB4715 927A 4A83 8F2A D09F99685E69.jpeg Straika Yanga atupia "Hat trick"

Thu, 7 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji chipukizi wa Yanga, Clement Francis Mziza amekuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat-trick kwenye Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20.

Nyota huyo alifunga mabao yote matatu akiisaidia timu yake kushinda 3-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi D usiku wa jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Mechi nyingine ya Kundi D jana, KMC ilitoa sare ya 1-1 na Kagera Sugar, wakati Kundi B, Mbeya Kwanza iliichapa 3-1 Ruvu Shooting na mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar wakaitandika 4-0 Dodoma Jiji.

Michuano hiyo ilianza juzi, Kundi A; Biashara United ikitoka sare ya 0-0 na Namungo FC na Simba SC ikaichapa Polisi Tanzania 2-1, wakati Kundi C, Tanzania Prisons iliichapa Coastal Union 1-0 na wenyeji, Azam FC wakaichapa Mbeya City 3-2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live