Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Yanga asubiriwa Ufaransa

Clement Francis Mzize.jpeg Clement Mzize

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera amesema anamuona mbali staa wa Yanga, Clement Mzize kutokana na juhudi anazoendelea kuzionyesha ndani ya timu hiyo huku akisisitiza kuwa bado ana nafasi ya kucheza soka nje ya nchi na atampambania.

Mzize akiwa na Yanga hadi sasa amefunga mabao sita na asisti moja, akifunga mawili na asisti moja kwenye Ligi Kuu Bara na amefunga mabao manne katika Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Yanga ilishapokea mualiko kutoka klabu kubwa ya Olympic Marseille ya Ufaransa wakimhitaji mchezaji huyo kwa ajili ya majaribio, baada ya kumuona mchezaji huyo katika mashindano ya soka la vijana chini ya miaka 20, ambapo alionyesha kiwango bora akifunga mabao 7 na kuwa mfungaji bora.

Akizungumza na Zahera raia wa Congo alisema mchezaji huyo ni hazina ya Tanzania miaka ijayo kutokana na kukosa wachezaji wa aina yake huku akisisitiza kuwa akiendelea na juhudi hizo haoni kama ataendelea kubaki ndani ya Yanga kwa sababu tayari ana ofa mezani.

Alisema kubaki Tanzania na kushindwa kwenda Olympic Marseille ya Ufaransa haina maana kwamba nafasi yake imepotea zaidi ameingia kwenye ufanisi ambao utamfanya aingie moja kwa moja kwenye timu hiyo na sio majaribio kama ilivyokuwa awali.

Alipotafutwa Mzize ambaye alisema imani anayoipata ndani ya kikosi cha Yanga kuanzia kwa wachezaji, benchi la ufundi, mashabiki na viongozi ni kubwa sana lakini ameomba kutopewa presha kwani bado ana safari ndefu.

“Siwezi kusema chochote kibaya au kizuri kwani bado nipo kwenye njia ya kujifunza. Nashukuru kwa kuaminiwa na kupewa nafasi.”

Chanzo: Mwanaspoti