Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Yanga amchana Mayele

Mayele Ambani Straika Yanga amchana Mayele

Thu, 21 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga Boniface Ambani amemshauri mchezaji wa Yanga na straika tegemeo wa timu hiyo Fiston Mayele kutobweteka na kuongeza juhudi kwani idadi yake ya magoli hairidhishi ukilinganisha na enzi zake wakati akiwa katika klabu hiyo.

“Nadhani amefunga zaidi ya bao kumi saizi lakini tuko mzunguko wa ngapi saizi? wa pili kwahivyo kidogo average scoring yake iko chini, wakati mimi nacheza Yanga timu zilikuwa 12 pekeyake sasa zipo 18 kwahiyo yeye mwenyewe kama Straika lazima aangalie Statistics zake asifunge bao moja tu akafurahi.”

Amedai pia kuwa enzi zile anacheza Yanga wachezaji wazawa walinufaika zaidi na ujio wa wachezaji wa kigeni kwani waliwapa vitu ambavyo wazawa hawakuwa navyo na wazawa kama kina Jerry Tegete, pamoja na Gaudence Mwaikimba.

Kwa upande mwingine Ambani amedai kama uongozi wa Yanga utaamua kumpa nafasi yoyote ile ndani ya klabu hiyo yupo tayari kurudi kwani alikuwa na wakati mzuri klabuni hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live