Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Yanga akimbia kero

Busungu Pic Data.png Straika Yanga akimbia kero

Fri, 19 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

STAA wa zamani wa Yanga aliyekuwa Lipuli, Malimi Busungu amefichua kuwa kutopenda kero na kuhofia kupata maradhi ya presha ndicho kilichomuondoa kwenye soka la ushindani mapema, ilhali bado hajaufanyia jambo la maana mchezo huo kama mchezaji.

Busungu aliyewika katika timu mbalimbali ikiwamo Mgambo JKT kabla ya kunyakuliwa na Yanga kisha kuibukia Lipuli, alisema aliamua kujiweka pembeni ili kujipa muda wa kujitafakari akitarajia kurejea upya aweze kukabiliana na changamoto hasa za mikataba ya kazi ambayo viongozi wengi hawafuati.

Akizungumza na Mwanaspoti, Busungu alisema aliachana na Lipuli baada ya kusubirishwa mshahara nje na makubaliano ya mkataba na kuona kwamba ili kuepuka gonjwa la moyo kwa mawazo ya kufikiria haki yake aliamua kujiweka nje ya uwanja na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji.

“Sipendi kujipa mawazo, napenda ukweli na ukiongea ukweli kuhusu kutafuta haki yako unaonekana ni mchezaji usiye na nidhamu, hicho ndicho kiliniondoa Lipuli, nimefanya kazi basi nipewe haki yangu, nilipoona siwezi niliondoka japo tulimalizana na kila mmoja anaendelea na yake,” alisema.

“Nasema hili kama mkombozi wa wachezaji wengi wenye kilio kama hicho, ila wanaogopa kuweka wazi kutokana na mifumo ya timu, kuhofia kuonekana mkorofi. Wapo watu waliondoka na wanazidai timu hadi leo na wana zaidi ya miaka hata 10, hii sio sawa ni jasho lao.”

Mbali na hilo, aliomba kila mchezaji angalau awe na mtu wa mpira wa kumjenga kiakili kwa kumuongoza namna gani anaweza akatunza kiwango chake kufika mbali, kitu anachoona kinakosekana ndio sababu ya wengi kupotea.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz