Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Simba aipigia hesabu Kagera Sugar

MOHAMED MUSSA Straika Simba aipigia hesabu Kagera Sugar

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Simba, Mohamed Mussa anayekwenda kucheza kwa mkopo wa miezi sita Kagera Sugar amesema ana matumaini ya kupata nafasi ya kucheza, akiamini atamaliza msimu huu kwa kwa kufanya kitu.

Simba ilimsajili Mussa kutoka Malindi ya Zanzibar, baada ya kufanya vizuri kwenye Kombe la Mapinduzi 2023, bao pekee alilofunga ni dhidi ya Coastal Union mechi ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Kwenye msimu huu hajacheza mechi hata moja ya Ligi Kuu kutokana na ushindani wa namba katika nafasi yake ila alicheza kwenye mechi za michuano ya Mapinduzi 2024 iliyofanyika Zanzibar, kitu kinachompa imani kupitia Kagera Sugar atarejesha kiwango chake.

"Naenda kucheza Kagera kwa mkopo, ingawa bado sijajiunga nao kwani kuna mambo hayajawekwa sawa, hivyo nasubiri kila kitu kiende kama tulivyopanga baina yangu na timu ninayokwenda kuichezea,"amesema na kuongeza;

"Kukosa namba Simba hakunifanyi nione ndio mwisho wangu wa kucheza, ndio maana wamenipeleka kwa mkopo, ili nikapata nafasi ya kucheza, huo ndio mpira wa miguu na mimi siyo wa kwanza."

"Natamani msimu huu, nirejeshe kiwango, ingawa natambua si kazi rahisi isipokuwa kwa kupambana bila kukata tamaa, inawezekana kabisa."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live