Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika: Shida ya Azam FC iko hapa

Azam Fcs Straika: Shida ya Azam FC iko hapa

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika wa zamani wa Kagera Sugar na Timu ya Taifa ya Tanzania, Philip Alando amesema kuwa tatizo la Klabu ya Azam lipo kwenye eneo la makipa kwani wamekuwa wakifanya makosa mara kwa mara yanayoigharimu timu.

Philip Alando amesema kuwa licha ya Azam kusajili vizuri karibu kila msimu lakini matokeo yao mwisho wa msimu yamekuwa hayaendi kama wanavyotarajiwa kutokana na eneo hilo la makipa kukosa mwarobaini tangu aondoke Aishi Manula mwaka 2017.

"Katika sehemu ambayo inaiangusha Azam kwa sasa ni pamoja na sehemu ya Goalkeeping. Unajua makocha wanapokuja kila kocha anakuwa na falsafa yake, kocha huyu kamtaka kipa huyu sasa kukawa lango halitulii, anaingia huyu anatoka huyu.

"Katika kipindi hiki ambacho ameondoka Razack (Abalora) na Aishi (Manula) kumepata kutokea magolikipa kama 3 hivi wa kimataifa, ukianza na Kigonya (Mathias ) Mganda yule naye amekuja lango halikuwa sawasawa, akaja Ahmada (Ali) naye tumeona alichokifanya bado lango halikuwa sawasawa.

"Amekuja Iddrisu (Abdulai) ambaye tunamuona ni much better kuliko hao wengine wawili waliopita lakini na yeye katika mechi zile ambazo unaamini sasa hili Iddrisu anatubeba basi hilo ndilo analokuangusha nalo," amesema Philip Alando, Meneja wa zamani wa Azam FC.

Katika mechi rasmi za mashindano tatu ambazo Azam imecheza tangu msimu huu umeanza, imeshinda mechi moja na kupoteza mechi mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live