Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Muivory aipasua Yanga

Yanga Pic 1 Data Straika Muivory aipasua Yanga

Fri, 18 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Mwandishi WetuMore by this Author KELELE za mashabiki wa soka hasa wale wa upande wa pili, wanaoiponda Yanga kwa kushindwa kupiga dozi ya maana kwenye mechi zao za Ligi Kuu Bara ni kama zimewaamsha mabosi wa klabu hiyo, ambapo kwa sasa akili zao ni kusuka kibabe safu yao ya ushambuliaji.

Katika kuonyesha kuwa mabosi hao wamepania hasa katika kuhakikisha msimu huu wanabeba ndoo waliyoitema misimu mitatu mikononi mwa watani wao, kwa sasa tayari mikononi mwao wana majina matatu ya washambuliaji katika meza yao na wote wakiwa na moto katika kufunga.

Hata hivyo, straika Muaivory Coast anaonekana kuwapasua zaidi kiasi cha mabosi hao kuanza kuchekesha akili kuhakikisha wanambeba kama mipango yao itaenda sawa.

Ripoti ya kocha Cedric Kaze inataka watu wasiozidi wawili katika dirisha hili dogo la usajili lililofunguliwa jana na mabosi wanapambana na mshambuliaji Gbagbo Junior Magbi.

Magbi yupo pale katika kikosi cha Mabingwa wa zamani wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Wydad Casablanca ya Morocco ambayo sasa ni kama inasuka upya safu yao ya ushambuliaji ikimnasa nyota wa kimataifa wa Tanzania, Saimon Msuva aliyetokea timu ya Difaa El Jadida.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz