Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Mtibwa kama Fei Toto

Adam Adam Adam Adam

Sun, 8 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati sakata la kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' jana likitolewa maamuzi na Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji, mshambuliaji nyota wa Mtibwa Sugar, Adam Adam ameandika barua ya kuvunja mkataba wake wa miezi sita uliobaki klabuni hapo.

Fei aliburuzwa na Yanga katika kamati hiyo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuvunja mkataba kwa kulipa Sh112 milioni ambazo hata hivyo zimerudishwa na jana maamuzi yalitoka na kuamuliwa bado ni mchezaji halali wa Yanga.

Lakini kwa Adam amewaomba waajiri wake kuvunja mkataba ili akatafute changamoto sehemu mpya na taarifa ambazo Mwanaspoti limepenyezewa na mtu wa karibu wa mchezaji huyo zilieleza kwamba ni kweli amefikia uamuzi huo ingawa bado viongozi wake hawajajibu chochote kuhusu hilo.

"Ni kweli anataka kutafuta changamoto kwenye timu mpya ingawa bado uamuzi wa mwisho juu ya hilo haujafanyika," kilisema chanzo hicho ambacho hata hivyo hakikutaka kuwekwa wazi.

Kwa upande wa Adam, alipotafutwa na Mwanaspoti alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa sasa.

"Kama kutakuwa na jambo lolote jipya ambalo linanihusu basi mashabiki wangu watajua tu," alisema.

Akizungumzia hilo, kocha msaidizi wa timu hiyo, Awadh Juma 'Maniche' alisema anaamini kila kitu kuhusu mchezaji huyo kitakamilika kwani wao kama benchi la ufundi bado wanamuhitaji.

Nyota huyo alijiunga na kikosi hicho akitokea Polisi Tanzania huku ikielezwa sababu kubwa ya kutaka kuvunja mkataba wake ni kwa ajili ya kujiunga na JKT Tanzania ambayo imemuwekea fedha nyingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live