Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Mpya Yanga asaini rasmi

69223 Pic+ndama

Fri, 2 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KLABU ya Yanga imemalizana na straika mpya kutoka Dr Congo, David Molinga 'Ndama' a.k.a Falcao baada ya kumsainisha mkataba jioni hii tayari kukipiga klabu hiyo ya Jangwani kwa mkopo kutoka Renaissance du Congo.

Klabu ya FC Renaissance ndiyo aliyokuwa akiichezea Heritier Makambo na kutua kwa Ndama kunaimarisha safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo sasa inaundwa na nyota wote wa kimataifa kutoka nje.

Mchezaji huyo anakuwa nyota wa 11 kusajiliwa Yanga, lakini tayari mabosi wa klabu hiyo wamemalizana na kipa Klaus Kindoki ili aondoke Jangwani kurejea klabu yake ya zamani ya Fc Lupopo ya DR Congo aliyokuwa akiichezea kabla ya kusajiliwa Yanga.

Kindoki alisajili kwa mkataba wa miaka miwili na ameutumikia msimu mmoja na ameridhia kurudi kwao DR Congo akipishana na Ndama aliyeifungia timu yake ya FC Renaissance mabao 11.

Kutua kwa straika huyo kunaifanya Yanga iwe na mastraika sita wa kigeni akiwamo Juma Balinya aliyesajiliwa kutoka Uganda, Mzambia Maybin Kalengo, Wanyarwanda Issa Bigirimana na Patrick Sibomana sambamba na Mnamibia, Sadney Urikhob.

Nyota wengine wa kigeni ni kipa Farouk Shikalo kutoka Kenya na mabeki Mghana Lamine Moro na Mrundi Seleman Mustafa.

Chanzo: mwananchi.co.tz