Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Mghana kutua Simba ni suala la muda tu

Opare Pic Data Collins Opare

Fri, 9 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba imeachana na Augustine Okrah, lakini kwa sasa inaelezwa ipo katika mazungumzo na Mghana mwingine anayekipita Dodoma Jiji, Collins Opare ambaye pia anatajwa kuwindwa na Singida Big Stars.

Opare aliyefunga bao pekee juzi usiku wakati Dodoma ikiizamisha Namungo nyumbani kwao katika mechi ya Ligi Kuu, ameonyesha kiwango cha hali ya juu msimu huu akiwa ametupia jumla ya mabao tisa, kiasi cha kuanza kunyatiwa na Simba na Singida kwa mechi za kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa mchezaji huyo aliyekuwa akiichezea Biashara United msimu uliopita kabla ya kutua Dodoma ni kwamba Opare amekuwa akifuatiliwa na mabosi wa Simba tangu akiwa na Biashara United, hivyo walitaka kuona muendelezo wa kiwango chake ili kujiridhisha naye.

Inaelezwa tayari ameshapigiwa simu na mabosi wa Simba kwa ajili ya mazungumzo tangu mapema kwenye dirisha dogo, lakini dili likakwama na sasa inaelezwa Simba imerudi upya, huku Singida ikiingilia kati dili hilo kutokana na kutaka kwao kukiimarisha chao kwa ajili ya msimu ujao.

"Tangu msimu uliopita Simba ilikuwa ikimtaka, ila ilitaka kuona kwanza kiwango chake, lakini kwa kasi aliyoionyesha msimu huu, imevutia mabosi hao na kurudi kwake wakizungumza na menejimenti yake, " kilisema chanzo hicho cha karibu cha Mghana huyo.

Hata hivyo, inaelezwa Opare ni kati ya wachezaji ambao wapo kwenye mipango ya benchi la ufundi la Singida chini ya Kocha Hans Pluijm. Nyota huyo raia wa Ghana, anatazamwa kuwa anaweza kumfanya kocha Pluijm kuwa na machaguo mengi.

"Kocha wetu (Pluijm anavutiwa naye (Opare) kwa sababu ni mchezaji mpambanaji na anayeweza kuendana na mbinu zake, kuhusu kufanya naye mazungumzo ni kweli tuliongea naye ila hakuna chochote ambacho kimefanya," kilisema chanzo makini kutoka ndani ya Singida na kuongeza;

"Tumegundua kuwa bado anamkataba na Dodoma wa mwaka mwingine mmoja, tutaangalia uwezekano wa kumsajili mwisho wa msimu maana pia alitueleza kuwa anaofa kutoka Simba na kama itashindikana itatubidi tusubiri wakati wa dirisha dogo," alisema mmoja wa viongozi wa Singida BS. Opare alipotafutwa kwanza alisema anafurahia namna ambavyo ameisaidia timu yake kuwa mbali na hatari ya kushuka daraja,

"Yalikuwa mapambano makubwa lakini jambo zuri ni kwamba tulipambana kama timu na kusogea nafasi za juu, bado tunamchezo mmoja mbele yetu baada ya hapo ndio tutaona nini kinafuata."

Alipoulizwa taarifa za kutakiwa na Simba, alisema kama mchezaji ni ndoto kucheza timu kubwa, japo aliliacha jambo zima kwa menejimenti yake kuona inakuwaje kwa msimu ujao.

Opare alisema hata wakati anakuja nchini na kujiunga na Biashara ndoto zake zilikuwa ni kuonwa kwanza kwa kiwango chake kisha kusaka maisha mazuri zaidi kwa klabu kubwa zikiwamo Simba, Yanga na Azam ambazo anaamini zina nafasi kubwa ya kumpaisha kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: