Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Mashujaa: Sina cha kujifunza kwa Jobe, yeye ndio ajifunze kwangu

Adam X Pa Jobe Straika Mashujaa: Sina cha kujifunza kwa Jobe, yeye ndio ajifunze kwangu

Mon, 8 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

“Sipendi kuangilia mechi za watu wengine, sina cha kujifunza, sasa nikajifunze kwa Jobe ? Mimi na Jobe nani ana magoli mengi hapa Tanzania ? Sasa kwanini nimuangalie Jobe ? Yeye labda ndo aniangalie mimi.

“Nikiangalia mpira inamaana najifunza ukiona sijaangalia siwezi kujifunza, kwasababu hakuna mtu nitamuangalia atanionesha kitu cha ziada katika huo mchezo.

“Lakini ipo michezo ambayo naiangalia, kwa mfano juzi nimeangalia mechi ya Arsenal kuna vitu najifunza, kwa hapa nyumbani kuna baadhi ya michezo naangalia Lakini kuwe na sababu, kama hakuna sababu naangalia movie,” Mshambuliaji wa Mashujaa FC, Adam Adam kwenye mahojiano na Ayoma Tv kuelekea mchezo wa Mashujaa dhidi ya Simba Sc, mchezo wa Kombe la Shirikisho la CRDB Benki utakao pigwa, Kesho Jumanne, Aprili 9, 2024 kuanzia saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live