Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Kagera Sugar asema vita bado

Anuary Jabir Bh Mshambuliaji wa Kagera Sugar, Anuary Jabir

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Kagera Sugar, Anuary Jabir amesema licha ya kutofunga bao lolote hadi sasa ndani ya kikosi hicho ila bado hajakata tamaa kwa sababu muda upo wa kutosha wa kurejea kwenye makali yake yaliyozoeleka.

Kauli ya nyota huyo imetolewa baada ya kutokuwa kwenye kiwango kizuri na timu hiyo msimu huu tangu aliporudi akitokea nchini Ubelgiji alikokwenda kwa ajili ya kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya KAA Gent.

“Ushindani umekuwa mkubwa ila kama nilivyosema hapo awali malengo yangu ni kuhakikisha kwanza timu inapata matokeo mazuri kwenye kila mchezo tunaocheza kisha hayo mengine ya kwangu binafsi yatafuata tu,” alisema.

Aidha, Anuary aliongeza bado michezo imebakia mingi na lolote linaweza kutokea hivyo anapenda kuona ushindani huu ukiendelea hadi mwishoni mwa msimu kwa sababu kwake inamuongezea motisha ya kuzidi kupambana.

Kwa upande wa kocha wa timu hiyo, Mecky Maxime alisema kutofunga kwa mchezaji huyo ni sababu inayomsumbua sana ila atakapoanza kufunga tu atarudi katika hali yake ya kujiamini kama ambavyo alifanya vizuri kwa msimu uliopita.

Msimu uliopita nyota huyo alimaliza na mabao matano ya Ligi Kuu Bara huku akiwa ndiye kinara ndani ya kikosi hicho.

Chanzo: Mwanaspoti