Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Ihefu ataka mabao 20

Amza Mshambuliaji wa Ihefu FC, Amza Mubarak Ngamchiya

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Ihefu FC, Amza Mubarak Ngamchiya aliyejiunga na klabu hiyo msimu huu 2023/2024 amesema anatamani kufunga mabao zaidi ya 20 kwenye Ligi Kuu Bara.

Rekodi ya kufunga mabao zaidi ya 20 mara ya mwisho kwenye Ligi Kuu ilifanywaa na aliyekuwa mshambuliaji wa Simba na sasa Singida Fountain Gate FC, Meddie Kagere msimu wa 2019/2020 aliyefunga magoli 22.

"Msimu huu natamani kufunga magoli 20 hata 25 pia inawezakana endapo kutakuwa na ushirikiano mzuri kati yetu sisi wachezaji benchi la ufundi na viongozi kwa ujumla, naamini nina kipaji na nilizaliwa kwaajili ya mpira,” amesema Ngamchiya na kuongeza;

"Nimejipanga kujituma zaidi msimu huu tunatakiwaa kujituma sote kama timu, nikipambana mwenyewe sitaweza kwasababu tuna cheza 11 uwanjani sichezi peke yangu,"

Ameongeza kuwa anafuraha na timu aliyopo kwa sasa timu iko vizuri ndio maana pia amejipanga kufanya vizuri zaidi ya misimu mingine aliyoitumikia Ligi kuu Bara

"Huku ni mbali na mjini sana lakini tunapata kila huduma, kiukweli nafurahia maisha haya na timu pia ipo vizuri"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: