Kiungo mshambuliaji wa Azam FC ambaye ni raia wa Gambia Gibril Sillah amesema Simba ina heshima kubwa katika mataifa mengine kutokana na miaka ya hivi karibuni kufanya vizuri kwenye mashindano ya klabu Afrika.
Gibril amesema kabla hajasajiliwa Azam akiwa na Raja Club Athletic ya Morocco ilikuwa ikitajwa Tanzania na wachezaji wengi walikuwa wanatamani kupata nafasi ya kuitumikia Simba kutokana na ushiriki wake na ubora waliokuwa wakionyesha katika mashindano hayo.
“Ilikuwa ikitajwa Tanzania, wachezaji wa mataifa mengi yalikuwa yanaitazama Simba kutokana na kufika hatua ya robo fainali mara nyingi, hiyo ilifanya baadhi ya mastaa wao kufuatiliwa kwa ukaribu,” alisema.
“Ndio maana ilikuwa rahisi kuwajua kina Clatous Chama, Luis Miquissone ambao walifanya vizuri kwenye michuano hiyo ukiondoa rafiki yangu Pape Sakho,” alisema mchezaji huyo.