Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Azam FC afunika Mapinduzi Cup

Allasane Diao I.jpeg Straika Azam FC afunika Mapinduzi Cup

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika wa Azam, Alassane Diao ameendelea kung'ara katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 baada ya kufunga bao la tatu hadi sasa huku akiongoza orodha ya wachezaji 11 waliochaguliwa kuwa nyota wa mechi (man of the match) mara nyingi hadi sasa.

Diao amelingana mabao na nyota wa Singida Fountain Gate, Elvis Rupia ambaye usiku wa jana alikuwa uwanjani kuikabili Simba kwenye mechi ya Kundi B, akiwa tayari amefunga mabao matatu katika mechi mbili za awali, lakini akichaguliwa mara mbili kuwa Nyota wa Mchezo na kuzoa kila moja Sh 500,000.

Katika mechi tatu ambazo Azam imeshacheza ikiwa Kundi A, Diao hakufunga mchezo wa kwanza dhidi ya Mlandege, kabla ya kufunga bao moja ilipoizamisha Chipukizi kwa bao 1-0 kisha jana akafunga mawili wakati Azam ikishinda 3-1 mbele ya Vital'O ya Burundi.

Katika mechi hizo zote alizofunga alichaguliwa Nyota wa Mchezo akiwa ndiye kinara kwani katika mechi 12 zilizopigwa hadi sasa hakuna mchezaji aliyechaguliwa mara mbili zaidi ya Diao, huku Azam ikitoa wachezaji watatu hadi sasa ikifuatiwa na Jamus iliyotoa wawili kama ilivyo kwa Singida.

Wachezaji hao wa Azam ni Yannick Bangala aliyekuwa mchezaji wa kwanza kabla ya Diao kufuatia mara mbili, huku Jamus ikiwatoa Benjamin Laku na Omer Michael, wakati Singida ikiwatoa Elvis Rupia na Morice Chukwu.

Klabu zilizotoa mchezaji mmoja ambao kila mmoja amevuna Sh 500,000 ni Suleiman Abrahman(Chipukizi), Akram Omar 'Haaland' (KVZ), Abdallah Kulandana (Mlandege), Crispin Ngushi (Yanga) na Fondoh Che Malone (Simba).

Mbali na nyota wa mchezo, Diao pia anaongoza orodha ya wafungaji akiwa sambamba na Rupia wa Singida, huku rekodi zikionyesha hadi sasa kwenye michuano hiyo kupitia mechi hizo 12 zilizopigwa jumla ya mabao 32 yamefungwa, likiwamo moja la kujifunga lilitumbukizwa wavuni na Mohamed Hassan (JKU) siku timu hiyo ilipovaana na Simba na kufumuliwa mabao 3-1.

Wachezaji wanaofuata kwa mabao baada ya Diao na Rupia ni; Akram Omar Muhina(KVZ), Crispin Ngushi (Yanga) na mfungaji Bora wa michuano hiyo kwa msimu uliopita, Francy Kazadi wa Singida kila mmoja akifunga mabao mawili na kufuatiwa na orodha ya wachezaji 19 waliofunga bao moja kila mmoja.

Orodha ya wafungaji;

3 Elvis Rupia (Singida FG)

Alassane Diao (Azam FC)

2 Akram Omar (KVZ)

Crispin Ngushi (Yanga)

Francy Kazadi (Singida FG)

1 Meddie Kagere (Singida FG)

Saleh Abdallah (JKU)

Optatus Lupekenya (Mlandege)

Kessy Nimubona (Vital'O)

Yussuf Mfaume (KVZ)

Yousif Mursal (Jamus)

Skudu Makudubela (Yanga)

Clement Mzize (Yanga)

Kibwana Shomary (Yanga

Moses Phiri (Simba)

Neva Kabona (JKU)

Saleh Karabaka (Simba)

Morice Chukwu (Singida FG)

Mbaoma Victor (APR)

Paschal Msindo (Azam)

Jean Nzeyimana (Vital'O)

Farid Musa (Yanga)

David Vicent (Jamus)

Nickson Kibabage (Yanga)

NB: Msimamo huu ni kabla ya mechi ya Jana ya Singida dhidi ya Simba

Chanzo: www.tanzaniaweb.live