Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steven Gerrard mrithi wa Dean Smith Aston Villa

Gerrard Villa Steven Gerrard ndie Kocha mpya wa Aston Villa

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aston Villa wamemteua Steven Gerrard kuwa Meneja mpya wa klabu hiyo akisaini mkataba wa miaka mitatu na nusu, na hivyo kuhitimisha uongozi wake wa miaka mitatu katika klabu ya Rangers.

Nahodha huyo wa zamani wa Liverpool, 41, anawaacha mabingwa hao wa Scotland akiwa amewaongoza kutwaa taji la kwanza la ligi katika kipindi cha miaka 10, msimu uliopita baada ya kuvunja utawala wa Celtic.

Gerrard anachukua nafasi ya Dean Smith, ambaye alitimuliwa Jumapili baada ya kupoteza michezo mitano mfululizo.

Villa wako katika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa EPL, pointi mbili juu ya eneo la kushushwa daraja.

"Aston Villa ni klabu yenye historia na utamaduni mzuri katika soka la England na ninajivunia kuwa kocha mkuu mpya," amesema Gerrard.

"Katika mazungumzo yangu na Nassef [Sawiris], Wes [Edens] na wengine wa bodi, ilionekana wazi jinsi mipango yao ilivyo kabambe kwa klabu na ninatazamia kuwasaidia kufikia malengo yao."

Gerrard aliichezea Liverpool michezo 710, akishinda mataji tisa, na aliondoka Liverpool mwaka 2015 ambapo alikwenda Ligi kuu ya Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live