Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steven Gerrard akutwa na Maambukizi ya uviko-19

Gerrard Steven Gerrard

Sun, 26 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa klabu ya Aston Villa Steven Gerrard atakosa michezo miwili ya ligi kuu ya Uingereza baada kupimwa kukutwa na maambukizi ya uviko-19, michezo ambayo ataikosa ni dhidi ya Chelsea leo siku ya boxing day na mchezo wa Jumanne watakao safiri kwenda Leeds.

Aston Villa mchezo wa wa wiki iliyopita dhidi ya Burnley ulihairishwa kutokana na visa vya wagonjwa wa korona kuzidi miongono mwa wachezaji, mchezo wao dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa Villa Park ni miongoni mwa michezo sita ya ligi kuu ya Uingereza ambayo itaandelea leo.

“Klabu ya Aston Villa imethibitisha kuwa kucha mkuu wa Steven Gerrard hataweza kuwepo kwenye michezo miwili inayofuata ya ligi kuu ya Uingereza ambayo ni Chelsea na Leeds united kwa sababu atapaswa kujitenga baada ya kukutwa na maambukizi ya Uviko-19.”

Michezo mitatu kati ya tisa leo imeahirishwa kutokana na visa vya wagonjwa wa korona kuzidi licha ya majeruhi kuwepo kwenye hizo timu. Steven Gerrad na aston villa yake mpaka sasa hawana uhakika wa mchezo wa tarehe 28 Disemba kwenye dimba la Elland Road kama utachezwa.

Michezo 25 ya siku ya leo barani Ulaya kwenye ligi kubwa nne imeahirishwa ukijumuisha na ligi zote za chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live