Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steven Gerrard aacha kazi Aston Villa baada ya kipigo

Stephen Gerr3.jpeg Steven Gerrard

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Club ya Aston Villa ya England imetangaza rasmi kuwa Kocha wake Mkuu Steven Gerrard ameacha kazi mara moja baada ya kipigo cha magoli 3-0 dhidi ya Fulham leo.

Taarifa za Gerrard kuacha kazi zimekuja saa moja baadae baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Fulham, Gerrard anaondoka Aston Villa baada ya kudumu kwa miezi 11 na siku 10 (11/11/2021-21/10/2022).

Gerrard anaondoka Aston Villa ikiwa nafasi ya 17 katika msimamo wa Ligi Kuu England yenye Timu 20 huku akiwa na alama 9 pekee alizovuna katika michezo 11, akishinda mechi 2, sare 3 na kupoteza game 6.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live