Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steven Gerrard: Ronaldo ameipaisha Saudi Arabia

Ronaldo Gerrard Steven Gerrard: Ronaldo ameipaisha Saudi Arabia

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Legendari wa Liverpool, Steven George Gerrard amesema kuwa Cristiano Ronaldo ndiye chachu ya maendeleo ya soka nchini Saudi Arabia.

Gerrard raia wa Uingereza anayefundisha Klabu ya Al-Ettifaq inayoshiriki Saudi Pro League, amesema usajili wa Ronaldo umewashawishi wachezaji wengi kujiunga na timu za Saudia na kuifanya Ligi hiyo kuwa maarufu na inayofuatiliwa zaidi Duniani.

“Nafikiri tangu alipo jiunga na Al-Nassar hapo Januari, mwaka huu The Goat (Ronaldo) kama tunavyomuita hakika ilikuwa ni dili kubwa kwake na bado amekuwa akihitajika na vilabu mbalimbali hadi sasa.

"Kwani Ujio wake ndani ya Ligi hii ameifanya iwe inafuatiliwa na Watu Wengi, huku ikifanikiwa Kusajili Wachezaji Wengi wa Kubwa kutoka Miongoni mwa zile Ligi 5 bora duniani," amesema Steve.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live