Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Steven Gerrard Muda Wowote kutua EPL

Gerrard Return Steven Gerrard

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Steven Gerrard ndie kocha anayepigiwa chapuo la kuchukua mikoba iliyoachwa na Dean Smith katika klabu ya Aston Villa kwa sasa, ni swala ka muda tu kupewa mikoba rasmi.

Aston Villa imekuwa ikitafuta mrithi wa kuinoa klabu hiyo tokea kumfurusha aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Dean Smith baada ya kichapo cha 1-0 kutoka kwa klabu ya Southampton.

Steven Gerrard amekuwa akipewa nafasi kubwa na kuwa chaguo la kwanza ambaye anaweza kuchukua mikoba hiyo, Gerrard amekuwa na uhusiano mzuri na mkuregenzi wa Aston Villa Christian Purslow tokea wakiwa wote Liverpool, ingawa Roberto Martinez, Paulo Fonseca, Kasper Hjulmand, Graham Potter na Ralf Rangnick nao wanapewa nafasi hiyo.

mafaniko ya Gerrard akiwa na klabu ya Rangers yamewavutia mabosi wa Aston Villa baada ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Scotland pasipo kupoteza mchezo wowote msimu ulioisha mbele ya mahasimu wao Celtics ambao walichukua ubingwa mara tisa mfululizo kabla ya Gerrard kufuta uteja huo msimu ulioisha.

Aston Villa kwa sasa inashika nafasi ya 16 ikiwa ina ponti 10 kwenye michezo 11 ya ligi kuu ya Uingereza “EPL” wakiwa wameshinda michezo mitatu, na kutoa sare mchezo mmoja, huku wakipoteza michezo saba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live