Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sterling kurudi Qatar bado kitendawili

Raheem Sterling Retrn Raheem Sterling

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raheem Sterling hatarejea kwenye kambi ya Uingereza Kombe la Dunia hadi familia yake iwe salama, na amewaambia marafiki kwamba anahitaji kuwa na ‘hakika ya asilimia 100’ kabla ya kurejea Qatar.

Nyota huyo ‘ametikisika’ kufuatia kuibiwa kwenye jumba lake la kifahari la Paundi Milioni 6, huku, huku akitajwa kuwa mchezaji wa nne wa Chelsea kulengwa na genge la hilo la uharifu.

Wezi walivamia nyumba hiyo kabla ya kuondoka na vito vya samani na saa, jambo lililomfanya nyota huyo aliyeshtuka kukimbilia nyumbani kwake akitoka Qatar ili kuwa na familia yake.

Polisi walitafutwa mwendo wa saa tisa alasiri siku ya Jumamosi, Desemba 3 baada ya mchumba wa Sterling, Paige kurejea na kukuta ‘idadi ya vitu vikiwemo vito na saa’ vimeibiwa.

Baadhi ya wachezaji wenzake wa Sterling wa Uingereza wanafahamika kuwa sasa wanakagua usalama wao wenyewe kutokana na tukio hilo la kuogofya.

Mwanasoka huyo, 27, anatarajia kurejea Qatar kwenye mechi ya robo fainali ya England dhidi ya Ufaransa Jumamosi, lakini atafanya hivyo ikiwa tu anahisi familia yake iko salama nyumbani kwao Surrey.

Raheem amewaambia kila mtu, “Hakuna njia ninaweza kwenda popote isipokuwa nina uhakika wa asilimia 100 kwamba familia yangu inaweza kuwekwa salama”.

Anajali usalama na sehemu ya sababu iliyowafanya kuhamia katika nyumba hiyo ni kwamba iko katika eneo la kipekee, na doria za mara kwa mara za usalama, chanzo kiliiambia The Sun.

Hata hivyo, Gareth Southgate hataweka shinikizo kwa Sterling kujiunga tena na kikosi cha Uingereza baada ya kurejea nyumbani kutokana na kushughulika na uchunguzi wa polisi kwa saa 48 zijazo.

Wafanyakazi wa Uingereza wanawasiliana na Sterling lakini Chelsea wanachukua nafasi ya uongozi akiwa Uingereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live