Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sterling kiroho safi kutua Man United

Rahemm Sterling United Sterling kiroho safi kutua Man United

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Winga wa Chelsea na England, Raheem Sterling, 29, yupo tayari kujiunga na Manchester United katika dirisha hili aidha kwa mkopo au mkataba wa kudumu lakini anataka kupokea mshahara sawa na ule anaoupokea sasa akiwa na matajiri hao wa Jiji la London.

Raheem ambaye mkataba wake umebakisha miaka mitatu kwa wiki anakunja kiasi kisichopungua Pauni 300,000 na ili aondoke kwa mkopo anataka mshahara huo usipungue hata kidogo.

Vilevile kama Chelsea itafikia makubaliano ya kumuuza mazima, anataka kuhakikishiwa kwamba anapokea mshahara sawa na ule wa sasa.

Sterling ni mmoja kati ya mastaa wa Chelsea walioondolewa katika kikosi cha kwanza na wamewekwa sokoni katika dirisha hili.

Msimu uliopita aliopita alionyesha kiwango bora akicheza mechi 43 za michuano yote na kufunga mabao 10.

Eddie Nketiah

KABLA ya dirisha kufungwa, mabosi wa Crystal Palace wana matumaini makubwa ya kukamilisha mchakato wa kumsajili straika wa Arsenal na England, Eddie Nketiah, 25.

Kwa mujibu wa ripoti Palace imekubali kutoa Pauni 25 milioni pamoja na nyongeza ya Pauni 5 milioni ambayo itatoka kwa kuzingatia kiwango atakachoonyesha.

Marc Guehi

NEWCASTLE inakaribia kukamilisha usajili wa beki wa Crystal Palace na England, Marc Guehi, 24, katika dirisha hili na taarifa kutoka tovuti ya Daily Mail zinaeleza dili hilo litaigharimu Newcastle kiasi kisichopungua Pauni 70 milioni.

Timu nyingi zilijaribu kumsajili staa huyu katika dirisha hili lakini zilishindwa baada ya Palace kushikilia msimamo wao wa kutaka Pauni 70 milioni kwa timu yoyote itakayomhitaji.

Matheus Nunes

ATLETICO Madrid inaangalia uwezekano wa kuipata saini ya kiungo wa Manchester City na Ureno, Matheus Nunes kwa mkopo wa msimu mmoja lakini hadi sasa haijaanzisha mazungumzo yoyote na matajiri hao wa Jiji la Manchester.

Nunes anataka kuondoka Man City kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Mkataba wake unamalizika mwaka 2028.

James Ward-Prowse

NOTTINGHAM Forest imepanga kuingia kwenye mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa West Ham, James Ward-Prowse, 29, ambaye kwa sasa sio sehemu ya mipango ya kocha mpya wa West Ham Julen Lopetegui.

Prowse ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliopita ni mmoja kati ya mastaa walioonyesha kiwango bora katika kikosi cha kwanza cha West Ham.

James Trafford

NEWCASTLE imerudi tena katika mazungumzo na Burnley kwa ajili ya kuipata saini ya kipa wa timu hiyo, James Trafford katika dirisha hili kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja ambao utakuwa na kipengele cha kumnunua mazima mwisho wa msimu.

Licha ya timu yake kushuka daraja msimu uliopita, James amekuwa mmoja kati ya mastaa wa Burnley wanaowindwa na timu mbalimbali za Ligi Kuu.

Alex Oxlade-Chamberlain

BRENTFORD imeingia katika mazungumzo na Besiktas kwa ajili ya kuipata huduma ya kiungo wa timu hiyo, Alex Oxlade-Chamberlain, 31, katika dirisha hili.

Mbali ya Brentford staa huyu ambaye ni raia wa England huduma yake pia inawindwa na Ajax.

Msimu uliopita Chamberlain alicheza mechi 30 za michuano yote na kufunga mabao manne. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.

Kingsley Coman

LICHA ya Arsenal na Manchester City kudaiwa kwamba zinahitaji kumsajili, kiungo wa Bayern Munich, Kingsley Coman anadaiwa kufikia makubaliano binafsi na Al-Hilal ya Saudi Arabia kwa ajili ya kujiunga nayo katika dirisha hili.

Coman mwenye umri wa miaka 28, anadaiwa kuomba kuondoka Bayern katika dirisha hili. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliopita alicheza mechi 27 za michuano yote.

Chanzo: Mwanaspoti