Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sterling akwepa kifungo EPL

Raheem Sterling Achunguzwa Raheem Sterling

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka nchini England (FA) halijamkuta na hatia yoyote mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Raheem Sterling baada ya kuwatupia kitu mashabiki wa Tottenham wakati wakishangilia goli la kusawazisha kwa timu yake lilifungwa na Palmer kwa mkwaju wa Penalty katika ushindi wa 4-1 dhidi ya majirani zao klabu ya Tottenham Hotspurs.

Sterling alionekana akichukua kitu uwanjani na kuwatupia mashabiki wa Tottehnham Hostspurs waliokuwa jukwaani.

Kitu hicho awali kilionekana kutupwa na mashabiki wa Totteham mapema kwa wachezaji wa Chelsea na kumgonga Palmer aliye isawazishia timu hiyo goli kwa mkwaju wa penalty.

FA wameliona tatizo hilo na wameamua kuwa hakuna haja ya kumfungia na kuendelea na kesi hiyo kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 28

Kama angepatikana na hatia basi Sterling angefungiwa. Mshambuliaji wa Tottenham Richarlson aliwahi kufungiwa mchezo mmoja wakati akiwa Everton kwa kutupa kitu jukwaani.

Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate amemuacha nyota huyo kwenye kikosi kitakachoshuka dimbani dhidi ya Malta na North Macedonia kwaajili ya kusaka tiketi ya kufuzu Euro 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live