Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sterling akubali yaishe England

Raheem Sterling Achunguzwa Sterling akubali yaishe England

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Chelsea na England, Raheem Sterling amekubali yaishe na kusisitiza anahitaji kuboresha kiwango chake ikiwa anahitaji kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England.

Kwa kipindi cha miaka saba, staa huyu amekuwa akiitwa timu ya taifa mara kwa mara, lakini hivi karibuni ameachwa mara tano na kuzua wasiwasi juu ya uwezekano wa kuitwa kwake kwenye fainali za Euro 2024.

Alipoulizwa kuhusu kuachwa kikosi cha England, Sterling alisema kwa sasa kitu pekee anachoweza kufanya ni kucheza vizuri uwanjani.

“Naweza kujaribu kuinua kiwango changu ili kurudi kwenye timu ya taifa kitu ambacho ndio nakipenda sana.”

Sterling amecheza mechi 55 za timu ya taifa England kati ya 82 chini ya Southgate, akiwa ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi chini ya kocha huyo baada ya Harry Kane, Harry Maguire, Jordan Pickford, Kyle Walker na John Stones.

Mechi yake ya mwisho kuonekana uwanjani akiwa na timu ya taifa ya England ni kwenye michuano ya Kombe la Dunia mchezo wa robo fainali dhidi ya Ufaransa mwaka 2022.

Kwenye Ligi Kuu England, maisha yake hayajawa mazuri sana tangu ajiunge na Chelsea akitokea Manchester City mwaka juzi na kiwango chake kimeshuka hali inayomlazimu kukirudisha ili Southgate afikirie kumrudisha timu ya taifa.

Chanzo: Mwanaspoti