Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sterling afikisha Mabao 100 EPL

Raheem Sterling Raheem Sterling akipiga mkwaju wa penati vs Wolves

Sun, 12 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raheem Sterling amerejea katika ubora wake sasa na alifanikiwa kufikisha mabao 100 ya Premier League baada ya kufunga kwa mkwaju wa penati dhidi ya Wolves siku ya Jumamosi.

Sterling anakuwa mchezaji wa 32 kufikisha idadi hiyo ya magoli kwenye Ligi ya Premia na 82 kati hayo amefunga akiwa na Manchester City na 18 alifunga akiwa na Liverpool.

“Ni mafanikio mazuri,” alisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27. “Kuna baadhi ya wachezaji wa ajabu katika orodha hiyo na nina heshima kubwa kuwamo sasa.”

Bosi wa City, Pep Guardiola aliongeza pongezi zake kwa mchezaji ambaye amepata shida kupata nafasi ya kikosi cha kwanza msimu huu baada ya kuchangia mataji yote ya awali ya City chini ya Pep.

“Katika umri wake, mabao 100 ni mengi,” alisema Guardiola. “Hongera kwake na timu. Raheem amekuwa muhimu kila wakati lakini wachezaji wanapaswa kuelewa hali ya juu na chini katika taaluma yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live