Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars yawasili Benin, Kim aanza mipango ya ushindi

Stars Benini (600 X 326) Kikosi cha Tanzania "Taifa Stars" wakiwasili nchini Benin

Fri, 3 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars jana jioni Alhamisi ya Juni 2 kilikwea pipa kuelekea nchini Benini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2023 dhidi ya Niger unaotarajiwa kuchezwa kesho Juni 4.

Leo Juni 3 tayari kikosi hicho kimewasili salama Benin ambapo mchezo huo ndipo utakapochezwa.

Benchi la ufundi limeweka wazi kwamba wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo muhimu na ambacho wanahitaji ni ushindi.

Stars ipo kwenye Kundi F ambapo kibarua chao wataanza dhidi ya Niger kesho kisha watarejea kwa ajili ya mchezo dhidi ya Algeria utakaopigwa Juni 8,mwaka huu 2022.

Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen amesema kuwa wanajua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kuweza kufanya vizuri.

“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu kutokana na ukweli kwamba tunakwenda kucheza nje ya nyumbani licha ya kwamba mchezo unachezwa Benin,lakini tunajiamini na maandalizi ambayo tumeyafanya tunapaswa kuanza kwa ushindi,” amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live