Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars yapokelewa kishua Ivory Coast

Taifa Stars Ivory Coast Stars yapokelewa kishua Ivory Coast

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' kimewasili salama nchini Ivory Coast kwa ajili ya kuanza kampeni zake kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Januari 13 hadi Februari 11.

Timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Adel Amrouche imetua nchini humo na jumla ya wachezaji 27 ambao wamepokelewa na vikundi mbalimbali vya ngoma ikiwa ni siku mbili tu zimepita tangu ilipocheza mchezo wa kirafiki na Misri na kupoteza mabao 2-0.

Stars iliyoweka kambi ya siku kadhaa Misri na kucheza mchezo huo wa kirafiki inatazamiwa kubeba matumaini ya Watanzania wengi licha ya kuangukia kundi gumu la 'F' lililokuwa na timu tishio Barani Afrika za Morocco, Zambia na DR Congo.

Tanzania inayoshiriki fainali hizo kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo 1980 na 2019 itaanza kampeni zake Januari 17 kwa kumenyana na Morocco, ikiwa ni mchezo unaosubiriwa kwa hamu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Laurent Pokou, San Pedro.

Baada ya hapo Stars itashuka tena kwenye uwanja huo huo wa Laurent Pokou Januari 21 kupambana na Zambia kisha kumalizia kundi hilo kwa kumenyana na DR Congo Januari 24, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly huko Karhogo.

Chanzo: Mwanaspoti