Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars yaondoka mifuko imenona

E38de68b431dd3c2c031ab71de1c0a4b Stars yaondoka mifuko imenona

Fri, 15 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imetoa Sh milioni 60 za posho za ndani za wachezaji wa timu ya taifa ya soka ‘Taifa Stars’ na bonasi ya mchezo wa kirafi ki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Fedha hizo ni sehemu ya mchango wake kusaidia maandalizi ya timu hiyo katika mashindano ya Chan 2021 yatakayofanyika Cameroon kuanzia kesho hadi Febuari 17.

Fedha hizo zilikabidhiwa kwa Nahodha wa Taifa Stars, John Bocco na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Abdallah Ulega katika hafla ya kuiaga timu hiyo iliyofanyika juzi katika Hotel ya Tiffany, Dar es Salaam, ambapo pia aliwakabidhi wachezaji Bendera ya Taifa.

"Serikali imechangia zaidi ya Sh milioni 60 kama bonasi na posho za ndani za wachezaji na benchi la ufundi, bado tunapambana kupata fedha ili kusaidia katika maeneo mengine, TFF hakikisheni mnasimamia nidhamu ya matumizi ya fedha hizi pamoja na nidhamu kwa vijana ili timu yetu iweze kutuwakilisha vyema," alisema Ulega.

Taifa Stars ambayo imepangwa Kundi D na timu za Zambia, Guinea na Namibia iliondoka jana kwenda Cameroon kwa ajili ya mashindano hayo. Tanzania itacheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Zambia ‘Chipolopolo’ Januari 19 utakaochezwa saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Stade Omnisports, wakati pazia litafunguliwa leo kwa wenyeji Cameroon `Simba Wasiofugika’ kucheza dhidi ya Zimbabwe kwenye Uwanja wa Ahmadou-Ahidjo kuanzia saa 10:00 jioni, kisha itacheza na Namibia Januari 23 na itamaliza michezo ya hatua ya makundi dhidi ya Guinea Januari 27.

Taifa Stars mara ya mwisho kucheza na Zambia ilikuwa kwenye mashindano ya COSAFA ambapo ilipoteza kwa mabao 4-2. Mataifa 16 yamepangwa katika makundi manne yenye timu nne kila moja. Kundi A Uwanja wa Ahmadou AhidjoYaoundé Cameroon, Zimbabwe, Mali, Burkina Faso Kundi B Japoma Stadium-Douala Libya, Niger, DRC, Congo Kundi C Uwanja wa Douala Morocco, Togo, Rwanda, Uganda Kundi D Uwanja wa Stade Omnisports Zambia, Tanzania, Guinea, Namibia

Chanzo: habarileo.co.tz