Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars yakubali kichapo kwa Mkapa

Stars Lost Winga wa Stars, Simon msuva akiwatoka Viungo wa Benin

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imetoka kichwa chini baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Benin katika mchezo wa makundi kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022

Katika mchezo huo ambao Stars waliutawala kwa asilimia kubwa, kipindi cha kwanza kilikua cha kucheza kwa kuviziana na mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko hakuna aliefanikiwa kuona lango la mwenzake.

Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko ambapo Stars walimtoa kiungo Novatus Dismas na kumuingiza mshambuliaji Kibu Denis.

Stars walifanya mashambulizi mengi ya hatari na kujikuta wanapoteza nafasi kwa kukosa utulivu kutoka kwa Simon Msuva na John Bocco.

Dakika ya 70 kukiwa kumeanzishwa mpira wa kawaida na walinzi zaidi ya watatu wakiwa eneo la Stars, Steve Mounie alipiga shuti la mbali lililotinga wavuni huku kipa Aishi Manula akiwa haamini kilichotokea.

Stars wakafanya mabadiliko kadhaa lakini hayakuleta mabadiliko na mpaka dakika 90 zinakamilika Benin wakaibuka na ushindi wa goli 1-0 ugenini. Katika mchezo mwingine wa kundi J, DR Congo imeibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya madagascar.

Kwa matokeo hayo Benin wanaongoza kundi J wakiwa na alama 7,wakifuatiwa na DR Congo yenye alama 5, na Stars imeporomoka mpaka nafasi ya tatu ikiwa na alama zake 4.

Stars itasafiri mpaka nchini Benin kukipiga katika mchezo wa marudiano Oktoba 10 huku wakijua ni lazima wapate ushindi ili waweze kuongoza kundi, huku wakimuombea DR Congo nae apoteze ama kusuluhu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live